Home news SIMBA YATOA TAMKO BAADA YA KUNYOOSHWA KWA MKAPA

SIMBA YATOA TAMKO BAADA YA KUNYOOSHWA KWA MKAPA


UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa utarejea ukiwa imara kwa ajili ya kuendelea na mapambano ndani ya uwanja kwa msimu wa 2021/22.

Jana, Septemba 25, Uwanja wa Mkapa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kesho Septemba 27 walipoteza kwa kufungwa baoa 1-0 dhid ya Yanga.

Ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa Tanzania na nje ya Tanzania.

Jitihada za Simba kupindua meza kuweka usawa mzani kwa bao lililofungwa na Fiston Mayele dakika ya 10 ziligonga mwamba kwa kuwa mbinu za Kocha Mkuu, Didier Gomes ziligoma.

Ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amebainisha kwamba watarejea wakiwa imara.

Barbara ameandika namna hii:”Every loss is a teachable moment.(kupoteza ni sehemu ya kujifunza) Tutarudi kwenye ubora wetu Insha’Allah!

SOMA NA HII  ALICHOKUWAFANYIWA NGASA NA YANGA...CHAMKUTA MAYELE...NI MWENDO WA SINDANO KILA MECHI...