Home Uncategorized KWA FEI TOTO, MKUDE ANAOMBA POO

KWA FEI TOTO, MKUDE ANAOMBA POO


 KIUNGO Jonas Mkude  wa Simba anaomba poo kwa rekodi kwa Feisal Salum, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga.

Kwa msimu wa 2020/21 Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 17, Fei ameanza kikosi cha kwanza mechi 15 na kukosekana kwenye mechi mbili huku Mkude ambaye timu yake imecheza jumla ya mechi 15 ameanza kikosi cha kwanza mechi 9.

Pia kwa upande wa nidhamu Fei ameonyeshwa kadi moja ya njano licha ya kucheza mechi nyingi akiwa amefunga bao moja kwa Mkude ambaye amecheza mechi chache zaidi ya Fei ameonyeshwa kadi mbili za njano kwenye rekodi zake na hajafunga bao wala kutoa pasi ya bao.

Pia Mkude amesimamishwa na Klabu ya Simba kwa kosa la utovu wa nidhamu ambapo anatarajiwa kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ili kujibu tuhuma ambazo zinamkabili kiungo huyo mzawa.

Mkude jumla ametumia dakika 814 uwanjani katika mechi 10 ambazo amecheza kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara alimaliza dakika 90 kwenye mechi 9 na mechi moja alitumia dakika 4.

Fei amemaliza dakika zote 90 kwenye mechi 13 ambazo ni daki 1,170 na mbili hakumaliza dakika 90 na kumfanya atumie jumla dakika 1,284 ndani ya uwanja.

Hizi hapa za Mkude Simba:-Ihefu FC dk 90Mtibwa Sugar dk 90Gwambina dk 4Prisons dk 90Ruvu Shooting dk 90Mwadui dk 90Kagera Sugar dk 90Yanga dk 90 mchezo huu alionyeshwa kadi ya njano mojaMbeya City dk 90 na KMC dk 90 ambapo pia alionyeshwa kadi ya njano moja.

Fei Toto ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons alitumia dk 90Mbeya City 60, Kagera Sugar 90, Mtibwa Sugar 90, Coastal Union 90,Polisi Tanzania 90, KMC 90.
Simba 90 na alionyeshwa kadi moja ya njano.

 Namungo 90, Azam FC 90, JKT Tanzania 54, Ruvu Shooting 90.Mwadui 90, Dodoma Jiji 90 na Ihefu 90 ambapo alipachika bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA ANGA ZA KIPA MRUNDI, ALIWABANIA YANGA