Home Uncategorized MZUNGUKO WA PILI UWE WA TOFAUTI, KOMBE LA SHIRIKISHO IWE NJIA KIMATAIFA

MZUNGUKO WA PILI UWE WA TOFAUTI, KOMBE LA SHIRIKISHO IWE NJIA KIMATAIFA


 MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa umeanza baada ya asilimia kubwa ya timu za hapa nyumbani kumaliza mzunguko wa kwanza.

Zimebaki chahe na viporo ambavyo inajulikana kwamba vimetokana na uwakilishi wa timu mbili ambazo ni Simba na Namungo kwenye michuano ya kimataifa.

Kukamilika kwa mzunguko wa kwanza bado kunabaki kuwa somo kwa timu ambazo zinapambana kwenye kivuli cha kushuka daraja.

Zipo zile ambazo hazijaweza kugusa ndani ya 10 bora tangu mzunguko uanze hapa kazi ipo kwa hizi timu kufanya tathimini ya kweli.

Ili uweze kubaki ndani ya ligi ya msimu huu ambayo ushindani wake ni mkubwa ni lazima uwe na nguvu ya kupambana na wale ambao wapo ndani ya 10 bora.

Ikiwa hakukuwa na mwendo mzuri kwa sasa ni muhimu kufanya maboresho kwani dirisha dogo la usajili bado linaendelea. Ninaamini kwamba usajili utazingatia matakwa ya mwalimu pamoja na benchi la ufundi.

Ukiachana na mwendelezo wa ligi pia kwa sasa kuna mashindano ya Azam Federation Cup ambapo yamerindima ikiwa ni hatua ya nne kwa timu kusaka tiketi ya kutinga hatua ya tatu.

Huku kwenye kila mchezo ni fainali ambapo ukipoteza safari yako inaishia hapohapo uliopoishia hivyo muhimu kujiweka sawa.

Kwa zile ambazo zimeishia njiani ikiwa ni pamoja na hatua ya tatu zinapaswa kujitafakari kwa ajili ya msimu ujao. Maisha yanakwenda kasi hivyo ni muhimu kwenda kwa kasi pia.

Tunaona kwamba wengi wamekuwa wakikata tamaa baada ya kushindwa kufikia malengo jambo ambalo halihitajiki kwenye ulimwengu wa mpira.

Huku bingwa anapewa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ni muhimu kujipanga kwa bingwa atakayepatikana.

Wale ambao wanapuuzia mashindano haya na kuishia njiani ni muhimu wakajua kwamba huku pia kuna faida.

Ushindani wa huku uzuri wake ni kwamba kila mechi ni fainali hivyo ukishinda mechi zako hakuna makelele wewe unateleza tu unakuwa wa kimataifa.

Nina amini kwamba wakati huu zile ambazo zimeishia hatua ya nne zitakuwa na picha ya kufanya kwa ajili ya wakati ujao na kuchukulia mashindano haya kwa uzito mkubwa.

SOMA NA HII  KUSHINDA KWA MBINDE KWA SIMBA SI UDHAIFU WA SVEN

Kila mmoja na kila timu ina nafasi ya kuwa washindi ikiwa itafanya maandalizi mazuri kwenye mechi ambazo watacheza hivyo bado kuna nafasi ya kujipanga.

Kwa zile ambazo zimetinga hatua ya nne ni muhimu kujipanga na kuleta ushindani wa kweli ili kupata matokeo mazuri.

Tunaamini kwamba mshindi wa kweli anapatikana kwa kila timu kuonyesha ushindani ndani ya uwanja. Kila timu na ipambane kwa hali na mali kupata matokeo chanya uwanjani.

Wakati ni huu na muda wa kupambana kwa yule bingwa lazima ajipange kufanya vizuri kimataifa ndani ya Kombe la Shirikisho.