Home Habari za michezo KISA CHELSEA KUVAMIA DILI LA KUMSAJILI JESUS…ARTETA ‘KIROHO JUU JUU’…AWALILIA MABOSI ARSENAL...

KISA CHELSEA KUVAMIA DILI LA KUMSAJILI JESUS…ARTETA ‘KIROHO JUU JUU’…AWALILIA MABOSI ARSENAL WAACHE UBAHILI…


Inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta hajapenda kuona timu hiyo ikienda kwa kasi ya taratibu kuwania kuinasa saini ya Gabriel Jesus.

Arteta ana hofu huenda akaikosa saini ya nyota huyo wa Manchester City ambayo ni muhimu kwake kwa ajili ya msimu ujao.

Usajili uliopita Arteta alitumia pauni milioni 150 kukamilisha usajili wa Ben White, Aaron Ramsdale na Martin Odegaard.

Kuelekea msimu ujao wa 2022/23 Arteta anahitaji kuimarisha zaidi kikosi chake ambacho kitashiriki Europa League na anahitaji kumsajili mshambuliaji ambaye ni Jesus.

Hofu ya Arteta kumkosa nyota huyo inatokana na dau ambalo linahitajika kutajwa kuwa ni pauni milioni 50 huku Chelsea na  Tottenham nazo zikitajwa kuwania saini ya mchezaji huyo.

SOMA NA HII  SAKATA LA MKATABA MPYA KWA FEI TOTO...EDO KUMWEMBE ACHOCHEA KUNI...AMCHANA GSM 'LIVE' BILA CHENGA...