Home Habari za michezo SAKATA LA MKATABA MPYA KWA FEI TOTO…EDO KUMWEMBE ACHOCHEA KUNI…AMCHANA GSM ‘LIVE’...

SAKATA LA MKATABA MPYA KWA FEI TOTO…EDO KUMWEMBE ACHOCHEA KUNI…AMCHANA GSM ‘LIVE’ BILA CHENGA…

Habari za Yanga

Baada ya kuanza msimu kwa kasi ya hali ya juu, Kiungo wa Kitanzania kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ameanza kupigiwa debe apewe Mkataba unaoendana na na kiwango anachoonesha.

Feisal ambae mara kadhaa amekuwa akiwapa Yanga matokeo kwa magoli yake ya kusisimua, Jana Disemba 4 katika Uwanja wa Mkapa kwa mara nyingine aliwapa Yanga alama tatu muhimu kwa bao lake la dakika za lala salama.

Sasa Mwandishi wa habari mwandamizi na mchambuzi wa Soka Edo Kumwembe kiaina amemshauri Feisal kudai maslahi zaidi katika mikataba yake na Yanga.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Edo ameandika;

“GSM wakishauza furniture sijui magodoro….mwishoni mwa msimu wampe Feisal hela inayoeleweka.

“Huwa nawashangaa akina Mpenja wanapomuita Feisal kama ‘Zanzibar Finest’….

“Fei kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi wa local eneo la kiungo kwenda mbele hapa kwetu achilia mbali mambo ya Zanzibar…one of the very best….uzuri ndani na nje ya uwanja anakuwa na furaha….”

Mkataba wa sasa wa Feisal unamalizika 2o24 huku kukiwa na tetesi za Matajiri wa Azam kumnyatia.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI