Home Uncategorized SIMBA NA YANGA KUKIPIGA MBELE YA RAIS MWINYI

SIMBA NA YANGA KUKIPIGA MBELE YA RAIS MWINYI

Jumla ya timu tisa ziwamo kutoka Tanzania bara na Zanzibar zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza mapema Januari 2021.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Omar Hassan (King) alibainisha hayo leo Desemba15, 2020 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari huko Maisara Mjini Unguja.

Alisema Kati ya timu hizo, timu tano kutoka Tanzania bara ikiwamo ni Simba, Yanga, Azam, Namungo na Mtibwa huku kutoka Zanzibar ni timu nne ikiwamo Jamhuri, Chipukizi, Mlandege na Malindi.

“Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Januari mosi au tatu, hiyo ni kutokana na utaratibu wa upangaji wa ratiba ya mashindano hayo, ” amesema King

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni Mtibwa ambaye alimfunga Simba bao 1-0 kwenye fainali iliyochezwa Januari 13, 2020 Uwanja wa Amaan.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA AZAM FC, NDAYIRAGIJE KUANZA NA HILI