Home Uncategorized SIMBA YAINGIA ANGA ZA KIPA MRUNDI, ALIWABANIA YANGA

SIMBA YAINGIA ANGA ZA KIPA MRUNDI, ALIWABANIA YANGA


 JONATHAN Nahimana, kipa namba moja ndani ya kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Hemed Morroco amewekwa kwa mara nyingine tena kwenye rada za mabingwa watetezi Simba ambao wanahitaji kuipata saini yake.

Simba chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck msimu uliopita wakati Nahimana anacheza ndani ya Klabu ya KMC wakati ikishinda mabao 2-0, kocha alisema kuwa kikwazo kilikuwa ni kipa huyo ambaye kwa sasa maisha yake yapo ndani ya Namungo.


Habari zinaeleza kuwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wameanza kumvutia kasi kipa huyo raia wa Burundi ambaye anacheza pia timu ya Taifa ya Burundi.


 Nahimana ambaye alikaa langoni kwenye mchezo dhidi ya Yanga Novemba 22 na kuizuia timu hiyo kusepa na pointi tatu wakati timu hizo zikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwa kuokoa michomo mitano ya moto kutoka kwa wachezaji wa Yanga amesema kuwa alifuatwa na mabosi wa Simba wakihitaji saini yake.


“Mimi ni mchezaji na nilikuwa nipo kwenye mazungumzo na Simba kabla ya kuja huku Namungo ila kabla mambo hayajawa sawa kuna mambo yalikwama ndio maana nipo Namungo.


“Kiukweli timu zote nilifanya nazo mazungumzo ya awali ikiwa ni pamoja na Simba ambao walinifuata mara mbili ila Yanga walinifuata mara moja, kwa sasa nasubiri dirisha dogo lifunguliwe nitajua itakuaje,” amesema.

Kwa sasa Namungo ina kibara cha kusaka ushindi mbele ya Al Rabita kwenye mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex Desemba 6 kwa sababu za kiusalama.


Mchezo wa kwanza Namungo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 hivyo inahitaji ushindi ili iweze kusonga hatua inayofuata na kipa huyo alikaa langoni na kuwazuia Wasudani kupata ushindi.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA:TUTAFUNGA MABAO MENGI KWA MIPIRA ILIYOKUFA