Home Uncategorized KAZE: UBINGWA YANGA UNAHITAJI SUBIRA, USHINDANI NI MKUBWA

KAZE: UBINGWA YANGA UNAHITAJI SUBIRA, USHINDANI NI MKUBWA


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anatambua shauku ya mashabiki pamoja na viongozi wa Yanga kwamba ni kutwaa ubingwa jambo ambalo anaamini linahitaji subira kutokana na ushindani kuwa mkubwa ndani ya Ligi Ku Bara.

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 13 kibindoni ina pointi 31 na imefunga jumla ya mabao 15 haijatwaa ubingwa kwa muda wa misimu mitatu mfululizo ambapo ubingwa ulikwenda kwa Simba.


Kwenye msimamo msimu wa 2020/21 inafuatiwa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi zake ni 26 baada ya kucheza mechi 13 na watani zao wa jadi Simba wapo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 11 na pointi zao kibindoni ni 23.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa anatambua shauku ya mashabiki ni kutwaa ubingwa baada ya kuukosa kwa muda mrefu jambo ambalo analipambania.

“Furaha ya mashabiki pamoja na viongozi ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ila bado tuna kazi ya kufanya kwa kuwa ushindani ni mkubwa ndani ya ligi.

“Kila timu ambayo tunakutana nayo ndani ya uwanja inapambana kupata matokeo kama ambavyo nasi tunapambana, bado tunaongoza ila haina maana kwamba kazi tumemaliza tutapambana ili kupata matokeo.


“Mashabiki wasiwe na presha kila kitu kinawezekana wao wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao,” amesema Kaze.


Mchezo uliopita Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, inakibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting, Desemba 6 Uwanja wa Mkapa.


Ruvu Shooting ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 23 sawa na wapinzani wa Yanga, Simba ambao wapo nafasi ya tatu tofauti ikiwa ni kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.


Simba imefunga mabao 29 baada ya kucheza mechi 11 na Ruvu Shooting imefunga jumla ya mabao 12 baada ya kucheza mechi 13.

 

SOMA NA HII  WAARABU WA MISRI WAPIDUA MEZA KIBABE MBELE YA SIMBA KWA NYOTA HUYU