Home Uncategorized SERGIO RAMOS BONGE MOJA YA BEKI NA MAKADI YAKE KIBAO KIBINDONI

SERGIO RAMOS BONGE MOJA YA BEKI NA MAKADI YAKE KIBAO KIBINDONI


SERGIO Ramos, beki anayekipiga ndani ya Klabu ya Real Madrid anatajwa kuwa miongoni mwa mabeki bora ambao wanacheza mpira kwa sasa duniani.

Beki huyo amekuwa kwenye ubora wake kwa muda mrefu huku ikielezwa kuwa yeye ndiye ameshika ufunguo wa ubingwa wa La Liga kwa msimu huu wa klabu hiyo ambayo inapambania kombe vikali na Barcelona.

Ndani ya uwanja amekuwa na rekodi nyingi nzuri ila mbali na kuwa bora ana rekodi ya kuwa mchezaji aliyeonyeshwa kadi nyingi uwanjani.

Kibindoni ana jumla ya kadi 187  ambazo ameonyeshwa kwenye maisha yake ya soka akiwa kwenye harakati za kupambana.


Ambapo ameonyeshwa jumla ya kadi 167 za njano na 20 nyekundu hiyo ni ndani ya La Liga pekee.

SOMA NA HII  YANGA YAINDIA ANGA ZA MTUPIAJI HUYU MZAWA