Home Habari za Yanga IMEFICHUKA RASMI…MCHEZAJI HUYU BONGO NI MCHUNGAJI…ISHU NZIMA A-Z

IMEFICHUKA RASMI…MCHEZAJI HUYU BONGO NI MCHUNGAJI…ISHU NZIMA A-Z

IMEFICHUKA RASMI...MCHEZAJI HUYU BONGO NI MCHUNGAJI...ISHU NZIMA A-Z

KAMA ulikuwa hujui kumbe kiungo wa Singida Big Stars, Bruno Gomes ni kama mchungaji ndio maana anapofunga bao hufunua jezi yake na kuonesha kwenye fulana yenye maneno yaliyomo kwenye Biblia.

Bruno ameonesha uwezo mkubwa wa kucheza nafasi tofauti uwanjani kwa ufanisi wa hali ya juu ambapo hadi sasa ametumika kama namba sita, nane, 10 na pia winga huku akifanya vizuri katika ufungaji wa mabao na kupiga pasi za mwisho.

Fundi huyo wa upigaji mipira iliyokufa, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao tisa huku akipiga pasi za mwisho nne katika michezo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ameifungia mabao mawili na pasi moja ya mwisho.

Kiungo huyo amekuwa akiwakuna mashabiki wengi kutokana na uwezo wake wa kupiga frikiki, kufunga na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Gomes kila anapofunga bao hukimbia kushangilia na kufunua jezi yake ambayo imeandikwa ujumbe mbalimbali mfano mchezo uliofanyika dhidi ya Mbeya City na ujumbe uliokuwepo ni ‘Nanyi mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru, Yohana 8: 32’

Msemaji wa timu hiyo, Hussein Massanza alisema Bruno ni kama mchungaji kulingana na matendo yake anayofanya uwanjani na nje ya uwanja.

“Ni kama mchungaji kwa sababu ya aina ya maisha anayoishi watu ambao hawafahamu kwanini nimemwita Bruno ni mchungaji, ni kutokana na maisha yake ni mchamungu sana hata machapisho mnayoyaona kupitia T-shirt zake unaona kabisa huyu ni mchungaji anaweza kukuwekea mkono na ukapata neema.

“Bruno ana namna yake ambayo anapenda kushangilia, kila siku anakuwa mbunifu mara ya kwanza katika T-shirt yake ilikuwa kwa lugha yao, mara ya pili kwa Kiingereza mara ya tatu ameamua kufanya kwa Kiswahili.

“Tunamsaidia kuhakikisha anafikisha ujumbe, ukiangalia haya yote ni maneno ya kwenye biblia anajaribu kusambaza injili hata kwenye michezo ni jambo jema,” alisema Msemaji huyo.
Katika hatua nyingine, Msemaji huyo alisema wamejipanga kwa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Yanga ama Geita inayotarajiwa kupigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Yanga na Geita zitacheza mchezo wa robo fainali ya ASFC keshokutwa Jumamosi mshindi atacheza na SBS.

“Sisi tunajiandaa kwa timu yoyote kwani timu zote zilizoingia ni ngumu hatutamani kukutana na timu yoyote lakini tunaamini tutakaekutana nae atakuwa ni mshindani mzuri, mashabiki wameona tunachokifanya, kujiamini kumeongezeka ingawa bado tuna kazi kubwa ya kufanya huko mbeleni hapa ndani ya nchi na mashindano Kimataifa, tunaomba waendelee kutupa ushirikiano,” alisema Massanza

SOMA NA HII  KIUNGO WA YANGA ATIKISA SHIRIKISHO...ALIKAA BILA TIMU NUSU MSIMU