Home Namungo FC NAMUNGO FC KAMILI GADO KUVAANA NA NKANA FC KWA MKAPA

NAMUNGO FC KAMILI GADO KUVAANA NA NKANA FC KWA MKAPA


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Nkana ya Zambia.

 

Mchezo huo wa tatu kwa timu hizo unatarajiwa kupigwa kesho Ijumaa, Aprili 2 katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Kwenye msimamo wa kundi D la michuano hiyo, Namungo inakamata nafasi ya tatu baada ya kupoteza michezo miwili ya kwanza.


 Walifungwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na kukubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

 

Ofisa Habari wa Namungo, Kindamba Namlia amesema: “Maandalizi yapo vizuri na tunatambua kwamba tuna kazi ya kufanya Aprili 2 mbele ya Nkana FC.

 

“Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wana morali kubwa ya kwa ajili ya kutafuta ushindi. Tupo nyumbani na tutatumia nafasi ya kuwa nyumbani kufanya vizuri,”.


Miongoni mwa nyota ambao wapo tayari kwa mchezo huo ni pamoja na Stephen Sey, Sixtus Sabilo, Shiza Kichuya, Humud.


SOMA NA HII  ILE ISHU YA KICHUYA KUTAKIWA TENA SIMBA...NAMUNGO WAIBUKA NA MADAI HAYA MAPYA...