Home Uncategorized MTUPIAJI SALIBOKO ACHEHELEA KUREJEA KWA LIGI

MTUPIAJI SALIBOKO ACHEHELEA KUREJEA KWA LIGI


DARUESH Saliboko, mshambuliaji wa Lipuli amesema kurejea kwa Ligi Kuu Bara kumempa furaha kutokana na kuukumbuka mpira kwa muda mrefu.

Hakukuwa na mechi ya ushindani tangu Machi 17 baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na kuibuka kwa janga la Virusi vya Corona ambalo linaitikisa dunia.

Kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo baada ya kueleza kuwa hali ya maambukizi imeanza kupungua nchini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema kuwa:”Muda mrefu hatukuwa na mechi za ushindani jambo ambalo limetufanya kwa pamoja tuukumbuke mpira.

“Kikubwa ambacho tunakisubiri kwa sasa ni muda wa kuanza kazi kwani kila kitu kipo wazi na kwetu ni furaha kuona kwamba tunarejea uwanjani,”.

Saliboko ametupia mabao nane ndani ya Lipuli akiwa nafasi ya pili ile ya kwanza ipo mikononi mwa Paul Nonga mwenye mabao 11.

SOMA NA HII  BEKI YANGA ATAKA KURUDI KMC, AGOMEA TIMU NYINGINE JUMLA