Home Uncategorized BEKI YANGA ATAKA KURUDI KMC, AGOMEA TIMU NYINGINE JUMLA

BEKI YANGA ATAKA KURUDI KMC, AGOMEA TIMU NYINGINE JUMLA


ALLY Ally, beki wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kuibukia kwenye Klabu yake ya zamani KMC  kwa mkopo na sio kwenda kwenye timu nyingine ikishindikana atabaki Yanga.

Ally alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha kubwa kwa kandarasi miaka miwili akitokea KMC, kwa sasa uongozi wa Yanga umepanga kumtoka kwa mkop kwenda JKT Tanzania jambo ambalo ameligomea.

“Sipo tayari kwenda kwenye timu nyingine kwa sasa, labda nirudi KMC hapo nipo tayari ila sehemu nyingine hapana siwezi kwenda,” amesema.

Jamila Mutabanzi, Ofisa Habar wa JKT Tanzania aesema kuwa Ally alipaswa ajiunge na wenzake kwenye mazoezi ila bado hajatokea.

“Tulipewa barua na Yanga kwamba wanataka aje kwetu kwa mkopo, suala la yeye kugoma hilo wanapaswa wamalizane ndani ya Yanga,” amesema.

SOMA NA HII  WINGA SIMBA ATUA YANGA KWA MILIONI 30