Home kimataifa MESSI AKUBALI KUKATWA MSHAHARA BARCELONA

MESSI AKUBALI KUKATWA MSHAHARA BARCELONA


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Barcelona, Lionel Messi yupo kwenye hatua nzuri ya kuongeza dili jipya ndani ya timu yake hiyo ambayo anaitumikia na amekubali kupunguza mshahara wake.

Nyota huyo ambaye ametoka kutwaa taji la Copa America baada ya timu yake ya taifa ya Argentina kushinda bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Brazil kwenye mchezo wa fainali, Uwanja wa Maracana, ambapo bao la ushindi lilifungwa na Angel di Maria ambaye ni kiungo anayekipiga ndani ya PSG.

Kwa sasa nyota huyo anajiandaa kusaini dili la miaka mitano kwa ajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo inayoshiriki La Liga, Hispania baada ya dili lake la awali kumeguka.

Mbali na kukubali kusaini dili hilo, Messi mwenye miaka 34 amekubali kukatwa mshahara kwa asilimia 50 kutokana na hali ngumu inayopitia timu hiyo kwa wakati huu kutokana na kuyumba kulikosasbabishwa na janga la Corona.

Kwa mujibu wa gazeti la ESPN, limesema kuwa mshambuliaji huyo amekubali kusaini dili jipya na kuwapiga chini Manchester United na PSG ambao walikuwa wanatajwa kuiwania saini yake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTAMBULISHWA RASMI LEO...KOCHA MPYA MAN UNITED KAFUNGUKA HAYA...