Home Uncategorized DUH!KUMBE ISHU YA KICHUYA NA SIMBA KUNA FILAMU ILIKUWA INACHEZWA

DUH!KUMBE ISHU YA KICHUYA NA SIMBA KUNA FILAMU ILIKUWA INACHEZWA


MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Simba,(CEO) Barbara Gonzalez amesema kuwa suala la Shiza Kichuya limesitishwa kwa kuwa Fifa walijua kwamba wanawasiliana na mtu ambaye hayupo ndani ya Simba.


Hivi karibuni habari zilieleza kwamba nyota huyo wa zamani wa Simba amefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita kutokana na kukiuka masuala ya usajili wake na Simba kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Kichuya ambaye alirejea ndani ya Simba akitokea Klabu ya Pharco ya Misri ambao inaelezwa kuwa waliishtaki Simba kwa kumsajili mchezaji akiwa bado na mkataba jambo ambalo liliwafanya Fifa kumpiga pini nyota huyo huku Simba ikitakiwa kulipa faini ndani ya siku 45.


Barbara kuhusu suala hilo amesema:-“Suala la Kichuya, Fifa wanatutendea haki. Tuliwaandikia na kuwaambia hatushirikishwa lolote na kulikuwa na mtu anawasiliana na Fifa nje ya klabu.


“Sasa tunasubiri barua ya Fifa kwa maana ya mashitaka na wametuandikia barua kuwa tuendelee na shughuli zetu, Shiza ni mchezaji huru na Simba inaweza kuendelea kusajili.


“Fifa nao waligundua waliyekuwa wanawasiliana naye si mtendaji wala kiongozi wa Simba na Kichuya unaona anaendelea hadi hapo tutakapopokea barua kutokea Fifa,” .


Kwa sasa Kichuya anaendelea na maisha yake ndani ya Klabu ya Namungo FC ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  ISHU YA YNGA KUVUKA MAKUNDI NJIA SAHIHI NI HII