Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO NA WASAUZI…RASMI…WACHEZAJI SIMBA WALA KIAPO CHA ‘MAANGAMIZI’….

KUELEKEA MECHI YA KESHO NA WASAUZI…RASMI…WACHEZAJI SIMBA WALA KIAPO CHA ‘MAANGAMIZI’….


Kiungo mkabaji wa klabu ya Simba SC mzamiru yassin amesema malengo yao kama wachezaji ni kuhakikisha wanafika nusu fainali kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika msimu.

Mzamiru amesema haya akiwa anazungumzia maandalizi ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini unaochezwa Jumapili Aprili 17, 2022. Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.

“Wengi wetu tulikuwepo mara mbili wakati tukiingia robo fainali lakini hatujawahi kufika nusu fainali, huu ndiyo wakati wetu kila mmoja yupo tayari. Sisi wenyewe morali yetu ipo juu na tupo tayari kutimiza malengo yetu,” amesema Mzamiru.

Hii ni mara ya tatu katika misimu minne Simba inafika hatua ya robo fainali, mara mbili zilizopita ilikuwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na mara zote waliondolewa katika hatua hiyo.

Kwa upande wa viongozi wa klabu hiyo nao wamekuwa wakinukuliwa kuwa malengo yao msimu huu ni kufika nusu faianali kama ikiwezekana wachukue kabisa ubingwa wa michuano hii.

SOMA NA HII  MCHONGO WA KING KIBA KUPERFORM LEO KUMBE FIFA WANAHUSIKA AISEE...ISHU IMEKAA HIVI...