Home news BAADA YA KUSHINDWA CAS…YANGA YAAMRIWA KUMLIPA MAMILIONI YA PESA MORRISON…

BAADA YA KUSHINDWA CAS…YANGA YAAMRIWA KUMLIPA MAMILIONI YA PESA MORRISON…


Mahakama ya Usuluhishi za Michezo Duniani (CAS) imeitaka Yanga kumlipa Bernard Morrison kiasi cha Swis Francs 5,000 (sawa na Sh12 milioni) ikiwa ni mchango wa kuendesha kesi ambayo Yanga imetupiliwa shauri lake walilokata dhidi ya mchezaji huyo wa Simba.

Yanga ilipinga uamuzi wa kamati hiyo ya TFF uliotolewa Agosti, 12,  2020  ambao ulikuwa ukieleza kwamba Morrison hakusaini nao mkataba ingawa ilithibitika kwamba Yanga ilimpa Dola 30,000 ambazo kamati ilimuamuru mchezaji huyo airudishie Yanga.

Kamati hiyo ilidai mkataba wa  Morrison ulimalizika Julai, 14,  2020. Hivyo kuanzia hapo alikuwa huru na mkataba wa mara ya pili wa Yanga haukuwa unatambulika.

Yanga ilipinga uamuzi huo wa TFF na kukata rufaa kwenda CAS wakiomba uhalali wa mkataba waliodai kwamba wamemsainisha kwa mara yapili na Morrison aamrishwe kulipa Dola 200,000 kama adhabu ya kusaini mkataba na Simba wakati bado alikuwa na mkataba na Yanga.

Baada ya rufaa  hiyo CAS kupitia taarifa yake iliyotoa leo imefafanua kwamba ilikaa kikao kwa njia ya video Julai mwaka huu na baada ya majadiliano imefikia uamuzi wa kuitulipilia mbali rufaa hiyo iliyowasilishwa na Yanga.

SOMA NA HII  KIMBUNGA CHA USAJILI CHANUKIA SIMBA....MBRAZILI APANIA KUIBOMOA VIPERS...MASTAA HAWA KUMFUATA...