Home Habari za michezo ALICHOKISEMA INJINIA HERSI BAADA YA YANGA KUPANGWA NA AL AHLY LIGI YA...

ALICHOKISEMA INJINIA HERSI BAADA YA YANGA KUPANGWA NA AL AHLY LIGI YA MABINGWA…

Habari za Yanga

Rais wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kukutana na wapinzani wao katika hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Young Africans imepangwa Kundi D sambamba na mabingwa watetezi wa Michuano ya hiyo Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana.

Rais huyo amesema kuwa wao wapo tayarı kukutana na wapinzani wao katika Kundi hilo, kwani hawaihofii timu yoyote zaidi ya wapinzani wao kuwa na kila sababu za kuihofia Young Africans kutokana na kuwa na kikosi bora na imara.

“Tumeshawafahamu wapinzani wetu katika hatua ya Makundi, timu yatu ipo tayari kupambana na yoyote katika Kundi D, kumbuka tuna timu nzuri ambayo inapaswa kuogopwa kutokana na ubora wake.

“Kitendo cha baadhi ya mashabiki kudhani tunaziogopa timu fulani, hilo halipo kabisa, kikubwa timu inapofanikiwa kutinga katika hatua ya makundi basi unatakiwa kuwa tayari kukutana na timu kubwa nyingine.

“Na ndio maana sisi tupo tayari kwa ajili ya kushindana na timu nyingine ambazo na zenyewe zimefanikiwa kufikia hatua hii ya makundi, ambacho tutajaribu kukifanya ni kuonyesha uwezo wetu kuhakikisha kuwa tunafanya vyema kwa kushindana na sio kwenda kushindwa,” amesema Hersi.

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ lilipanga Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani humo msimu huu 2023/24, huku mchaka mchaka kwa timu shiriki katika hatua hiyo ukitarajiwa kuanza Novemba 24.

CAF ilipanga makundi hayo mjini Johannesburg-Afrika Kusini juzi Ijumaa (Oktoba 06), chini ya Mkuu wa Idara ya Mashindano ya Shirikisho hilo, Khalid Nassar.

Makundi mengine katika MIchuano hiyo: Kundi A: FC Nouadhibou, TP Mazembe, Mamelodi Sundowns na Pyramids Kundi B: Simba ASEC Mimosas, Jwaneng Galaxy na Wydad AC Kundi C: Espérance de Tunis, Étoile du Sahel, Petro de Luanda na Al Hilal

SOMA NA HII  MWAMBUSI AKABIDHIWA YANGA MAZIMA, MCHAKATO WA KOCHA MPYA UMEFIKIA HAPA