SUDY Dondola, mlinda mlango namba moja wa Coastal Union amesema kuwa kupoteza pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkwakwani chanzo alikuwa yeye jambo linalomuumiza.
Coastal Union ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao la usiku lililopachikwa na Graham Naftar dakika ya 90 na lile la kusawazisha bao la Coastal Union lililofungwa na Mudhathir Said dakika ya 50 lilifungwa na Sadat Mohamed dakika ya 77.
“Nilikuwa na kazi kubwa ya kulinda lango letu ili tushinde ia mwisho wa siku hesabu zilinigomea jambo ambalo linaniumiza, ninaomba radhi kwa mashabiki wa timu yangu ya Coastal Union.
“Mimi ni mlinda mlango namba moja ninatakiwa kuwa makini muda wote, nimejifunza kupitia makosa na kupoteza Mkwakwani mbele ya mashabiki wetu inauma,” amesema.