Home Uncategorized JAMES KOTEI AZUNGUMZIA ISHU YAKE NA YANGA, KILICHOMKUTA KAIZER CHIEFS ACHA KABISA

JAMES KOTEI AZUNGUMZIA ISHU YAKE NA YANGA, KILICHOMKUTA KAIZER CHIEFS ACHA KABISA


KIUNGO bora ndani ya klabu ya Simba msimu wa mwaka 2018/19 James Kotei ambaye alitimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini amekubaliana kuvunja mkataba na klabu hiyo huku akisema kuwa hakuwa na furaha ndani ya timu hiyo.

Kaizer Chief wamefikia hatua hiyo baada ya kumpata mbadala wake kutokana na Kotei kutokuwa na nafasi ndani ya kikosi hicho.

Kotei amesema kuwa alikuwa hapati namba kikosi cha kwanza na hakuwa na furaha ndani ya timu hiyo kutokana na hali hiyo kwani furaha yake ipo kwenye kucheza.

“Sikuwa na furaha kwa kuwa nilikuwa sipati namba, natarajia kupata timu hivi karibuni ila sijazungumza na Yanga jambo lolote kuhusu wao kuhitaji saini yangu,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA YA GSM NI MOTO WA KUOTEA MBALI.. VIFAA VIPYA KUTOKA CONGO NA KENYA VYANUKIA JANGWANI