Home Uncategorized AZAM FC KAZINI TENA EO MBELE YA LIPULI, TAIFA

AZAM FC KAZINI TENA EO MBELE YA LIPULI, TAIFA

ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC  leo ana kazi nzito mbele ya Lipuli FC kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli utakaochezwa Uwanja wa Taifa, saa 1:00 usiku.

Cioaba ametoka kupoteza kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa kwa penalti 3-2 na Simba kwenye mchezo wa nusu fainali baada ya dakika tisini kutoshana nguvu ya dakika 90. 

Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu wanasahau masuala ya mapinduzi.

Azam FC imesajili wachezaji wawili dirisha dogo ambao ni kiungo Khleffin Hamdoun aliyepewa kandarasi ya miaka minne kutoka Mlandege ya Visiwani Zanzibar na Never Tigere aliyetoka Platinum ya Zimbabwe.
SOMA NA HII  WACHEZAJI SABA WA SIMBA WANAOPEWA NAFASI YA KUSEPA MSIMU UJAO