Home Uncategorized TOTTENHAM WABISHI KWELI, WAIGOMEA MKWANJA WA INTER MILAN NA KUWAPA MASHARTI MENGINE

TOTTENHAM WABISHI KWELI, WAIGOMEA MKWANJA WA INTER MILAN NA KUWAPA MASHARTI MENGINE


UONGOZI wa Tottenham umeigomea timu ya Inter Milan kumpata nyota wake Christian Eriksen ambaye yupo kwenye mpango wa kutimka ndani ya kikosi hicho.
Tottenham iliyo chini ya Jose Mourinho imekataa dau la pauni milioni 10 ambalo liliwekwa mezani na mabosi hao ili kuipata saini ya mchezaji huyo.
Licha ya mkataba wa kiungo huyo kufika ukingoni mwishoni mwa msimu bado haijawapa presha kubwa mabosi wa Tottenham wamekomaa na kuhitaji mara mbili ya dau hilo hivyo Inter Milan wanatakiwa waweke mezani pauni milioni 20 ili wafikiriwe kumpata nyota huyo.

Ericksen jana alianza kwenye kikosi kilichoshinda mabao 2-1 kwenye mchezo wa FA mbele ya Middlesbrough ambapo mabao ya ushindi yalifungwa na Glovan Lo Celso dakika ya pili na Erick Lamela alipachika bao la pili dakika ya 15 huku ile la kufutia machozi kwa Middlesbrough likifungwa na George Saville
SOMA NA HII  VIDEO:HIKI NDICHO ALICHOZUNGUMZA SHABIKI WA YANGA MBELE YA OFISA HABARI WA SIMBA HAJI MANARA