Home Habari za michezo INJINIA HERSI: MASHABIKI YANGA WANATUKOSEA SANA…WANATUVUNJA MOYO…

INJINIA HERSI: MASHABIKI YANGA WANATUKOSEA SANA…WANATUVUNJA MOYO…

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said

Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Saidi amesema pamoja na timu kukosa ushindi dhidi ya Club African katika mchezo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika lakini bado haijakata tamaa.

Hersi amesema wachezaji pamoja na benchi la ufundi walitumia kila mbinu ndani ya uwanja lakini ilishindikana na kwamba bado wana matumaini ya kufanya vizuri katika mechi ya marudiano.

β€œNimeona maoni mengi ya mashabiki wetu wakitupia lawama benchi la ufundi, wachezaji na hata viongozi, wanakosea hiyo ni kuwavumja nguvu wachezaji. Wachezaji na benchi la ufundi walipambana, naamini haikuwa bahati kwetu ila tunazo dakika 90 nyingine za kujiuliza,amesema Hersi.

Amesema kinachofafanyika hivi sasa ni kuiandaa timu kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili kutimiza lengo la kucheza hatua ya makundi ingawa amekiri kuwa mchezo utakuwa mgumu.

Club Africain itaikaribisha Yanga katika mchezo wa marudiano Tunisia Novemba 9, 2022.

SOMA NA HII  BAADA YA KUOTEWA NA SIMBA JUZI....HIZI HAPA MECHI KOKI ZA YANGA SC ZILIZOBAKI...WAKIFELI NDIO BASI TENA...