Home Habari za michezo KISA KIPIGO CHA GOLI 5 BILA KUTOKA SIMBA….KOTEI AIBUKA NA HAYA MAPYA...

KISA KIPIGO CHA GOLI 5 BILA KUTOKA SIMBA….KOTEI AIBUKA NA HAYA MAPYA MTIBWA SUGAR…

Licha ya kupokea kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba, kiungo James Kotei amesema Mtibwa Sugar inaonyesha mwanga wa kufanya vizuri msimu huu kulinganisha na ule uliopita walioponea chupuchupu kushuka daraja.

Kotei anayecheza kwa mkopo Mtibwa Sugar akitokea Singida Big Stars, alisema uwepo wa nyota wenye kiwango bora katika kikosi cha timu hiyo umeifanya iwe na uhakika wa kupata matokeo mazuri katika mechi nyingi za ligi msimu huu na kujiweka katika uwezekano mkubwa wa kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo.

“Tumesikitika kupata matokeo mabaya dhidi ya Simba, lakini soka ndio liko hivyo. Kuna nyakati unaweza kujipanga vizuri na mambo yakaenda ndivyo sivyo, hivyo kama timu tunapaswa kusahau kwa haraka kilichotokea na kujipanga na michezo inayofuata.”

“Ukikitazama kikosi chetu na jinsi tulivyoanza ligi, unapata imani tuna timu nzuri ambayo ina nafasi kubwa ya kumaliza nafasi nne za juu. Nina furaha kuwepo ndani ya Mtibwa japo kwa mkopo kutokana na mazingira bora niliyokutana nayo hapa,” alisema Kotei.

Kotei alisema ushindani wa ligi msimu huu unawalazimisha kuhakikisha hawapotezi pointi kirahisi jambo ambalo litawafanya waporomoke kutoka nafasi ya nne waliyopo sasa kwenye msimamo wa ligi.

“Tunapaswa kuendeleza mwanzo mzuri tulionao. Kupoteza dhidi ya Simba hakutakiwi kututoa kwenye reli na badala yake kituamshe mechi zinazofuata. Ligi imekuwa na ushindani hivyo salama pekee ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu kwani hatutaki kurudia makosa yaliyowahi kujitokeza nyuma,” alisistiza kiungo huyo.

Katika mechi 10 ilizocheza msimu huu, Mtibwa Sugar imekusanya pointi 15, ikipata ushindi katika mechi nne, kutoka sare tatu na kufungwa mbili huku ikipachika mabao 12 na kufungwa mabao 16.

SOMA NA HII  HUKU MKATABA WAKE UKIWA UKINGONI...KIBWANA SHOMARY ASHINDWA KUJIZUIA YANGA...AFUNGUKA HAYA...