Home Uncategorized MLINDA MLANGO YANGA: WASHAMBULIAJI WOTE BONGO WAPO VIZURI

MLINDA MLANGO YANGA: WASHAMBULIAJI WOTE BONGO WAPO VIZURI


MLINDA mlango namba mbili wa Yanga, Metacha Mnata amesema kuwa washambuliaji wote Bongo wapo vizuri ila kinachohitajika kwa mlinda mlango ni umakini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mnata amesema kuwa kwenye kila mechi kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa alikuwa anakutana na ugumu kutoka kwa washambuliaji jambo ambalo lilikuwa linamfanya apambane kuwa bora.

“Kila mechi ina changamoto zake na ushindani wake ambao unapatikana kutoka kwa washambuliaji ambao wanacheza ila mwisho wa siku kazi ya mlinda mlango ni kuzuia hatari.

“Ni ngumu kuwa bora muda wote hasa michomo inapozidi kuwa mikali hivyo ili kujilinda inatakiwa kuongea na mabeki wazidi kuwa makini, pale wanapoongeza umakini ni nafuu kwa mlinda mlango pia kuwa bora,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI