Home Habari za michezo BABA MZAZI WA FEI TOTO AINGILIA SAKATA LA MTOTO WAKE KURUDISHWA YANGA…MSIMAMO...

BABA MZAZI WA FEI TOTO AINGILIA SAKATA LA MTOTO WAKE KURUDISHWA YANGA…MSIMAMO WAKE HUU..

Tetesi za Usajili Yanga

Baba Mlezi wa Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, amesema wanaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, japo wanaamini kuna mahala wanaweza kupata haki ya mtoto wao.

Mzee Ally, Baba Mlezi wa Feisal amesema: “Mtoto yuko nyumbani amepumzika. Kama wazazi hatuna la kuzungumza kwa sasa tunawaachia Wanasheria wetu. Haki ipo na CAS watatupa majibu sahihi.

“Lakini kama kuna uwezekano wamuachie mtoto aende sehemu anayoitaka. Kurudi Yanga au kutorudi, binafsi sijui. Maamuzi yako kwake na siwezi kumuingilia”

Uongozi wa Yanga uliwasilisha Malalamiko mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ukidai Mchezaji huyo ametoroka kambini sambamba na kuvunja Mkataba kinyume na utaratibu.

Mwishoni mwa juma lililopita Feisal alitakiwa kurejea Young Africans baada ya kuthibitika Mkataba kati yake na Klabu hiyo ni halali na unatambulika kisheria.

SOMA NA HII  YANGA ILITUPIGA KIPIGO CHA MBWA KOKO...WANGETUONEA HURUMA TU...SISI HATUPO LIGI YA MABINGWA