Home news KAGERE AOMBA KUONDOKA SIMBA, YANGA WAANDAA MKATABA

KAGERE AOMBA KUONDOKA SIMBA, YANGA WAANDAA MKATABA


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Simba, Meddie Kagere amewasilisha kwa uongozi wa Simba barua ya maombi ya kutaka kusitisha mkataba wake ndani ya klabu hiyo kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, huku ikielezwa kuwa muda wowote huenda akajiunga na Yanga ambayo imekuwa ikimnyemelea.

Kagere amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Simba msimu huu, kutokana na ushindani mkubwa wa namba kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo hasa kutokana na usajili wa Straika, Chris Mugalu.

Kwa muda wa misimu mitatu ambayo Kagere ameichezea Simba kwenye Ligi Kuu Bara pekee Kagere amefanikiwa kuifungia Simba mabao 58, kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara pekee, ambapo msimu wa 2018/19 alifunga mabao 23, 2019/20 mabao 22 na msimu wa 2020/21 mabao 13.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba kimefunguka kuwa, Kagere alikutana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji juzi Jumanne usiku, ili kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

“Ni kweli Kagere amekutana na bosi MO, kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kufikia makubaliano ya pande zote mbili na kuachana na Simba, hii ni kutokana na mchezaji huyo kuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya klabu ya Simba.” kimesema chanzo hicho.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu kuzungumzia suala hilo amesema: “Kwangu binafsi nisingependa kuliongelea suala ambalo bado halijafanyiwa uamuzi na bodi ya Wakurugenzi, subiri mpaka tutakapokaa na kufikia uamuzi na tutatoa taarifa.”

Shangwe limehamia Kwa upande wa Yanga ambapo moja Kati ya viongozi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema: “Msimu huu lazima tutawashangaza watu kwa kusajili mchezaji mkubwa kutoka katika moja ya Klabu kubwa Tanzania, jambo ambalo linaashiria huenda akawa ni Meddie Kagere,” amesema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  TFF 'YAIBA' TUZO ZA LUIS MIQUISONE NA CHAMA....BOCCO NA 'FEI TOTO' WATAJWA