Home Simba SC BAADA YA CHIKWENDE, MAJEMBE HAYA MATANO YAPO KWENYE HESABU ZA SIMBA

BAADA YA CHIKWENDE, MAJEMBE HAYA MATANO YAPO KWENYE HESABU ZA SIMBA

BAADA ya mabosi wa Simba kukamilisha usajili wa nyota wa Klabu ya FC Platinum, Perfect Chikwende sasa inatajwa kuwa nyota wengine watano wapo kwenye rada za kutua ndani ya kikosi hicho.

Nyota anayetajwa kumalizana na Simba ambayo kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Seleman Matola ni kiungo wa DC Motema Pembe, Karim Kiekie.

Nyota huyo anakipiga pia kwenye timu ya Taifa ya Congo na yupo na timu ya Taifa ya Congo ambayo inashiriki michuano ya Chan.

Anatajwa kuwa miongoni mwa vijana wanaofanya vema ndani ya uwanja kwa uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto.

Mwingine anayetajwa kuwekwa kwenye rada za Simba ni pamoja na Peter Mudawa raia wa Zimbabwe ambaye anacheza ndani ya Klabu ya Highlanders.


Na mshambuliaji raia wa Nigeria Junior Lukosa naye anatajwa kumalizana na mabosi hao kilichobaki ni suala la kutambulishwa 

Mbali na nyota hao watatu pia kiungo mwingine ambaye anatajwa kuwa kwenye rada za Simba ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni pamoja na Nomore Chinyerere ambaye ni kiraka ndani ya kikosi cha FC Platinum ambapo alikuwa anakipiga na kiungo mwenzake Chikwende ambaye yupo zake ndani ya Simba.
Nyota wa tano ni mzawa Abdulmajid Mangalo ambaye yupo zake ndani ya kikosi cha Biashara anatajwa kuhitajika na mabosi hao.
Lengo la maboresho ya kikosi hicho ni kuona kwamba timu hiyo inaweza kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa timu hiyo ni imara na itafanya mambo makubwa katika usajili.

“Kuhusu usajili suala hilo lipo mikononi mwa benchi la ufundi ikiwa kuna wachezaji ambao watakuwa wanahitajika basi tuna amini kwamba tutawapata na tutafanya nao kazi kama benchi la ufundi litakubali,”. 
SOMA NA HII  HII HAPA MASHINE YA KAZI KUTOKA ASEC MIMOSAS INAYOKUJA YANGA...SHABANI DJUMA ATAFUTE PAKWENDA..