Home Uncategorized SEPETU: WACHEZAJI WALITUANGUSHA AFCON, LEO HAPANA, MASHABIKI TUJITOKEZE

SEPETU: WACHEZAJI WALITUANGUSHA AFCON, LEO HAPANA, MASHABIKI TUJITOKEZE

WEMA Sepetu, shabiki mkubwa wa timu ya Taifa ya Tanzania na mjumbe wa kamati ya uhamasishaji wa timu ya Taifa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa leo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania na Kenya huku akiwataka wachezaji wasiliangushe Taifa.

Sepetu amesema kuwa alipata furaha kubwa timu ilipofuzu michuano ya Afcon ila iliyeyuka kama barafu baada ya wachezaji kuboronga nchini Misri.

“Nilifurahi sana nilipoona timu ya Taifa letu imefuzu michuano ya Afcon ila sasa walipofuzu sijui bahati mbaya sijui ilikuaje walituangusha sasa katika hili basi wasituangushe hawa kaka zetu.

“Ninajua watanzania wanapenda mpira hivyo tujitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu ya Taifa na ombi langi kwa wachezaji wasituangushe,” amesema.

Stars leo itashuka uwanja wa Taifa kumenyana na timu ya Kenya majira ya saa 10:00 jioni.

SOMA NA HII  SIMBA YAWAITA MASHABIKI WAKE UWANJA WA TAIFA LEO