Home Uncategorized MWANAMICHEZO AZIM DEWJI AZIDI KUTENGAMAA

MWANAMICHEZO AZIM DEWJI AZIDI KUTENGAMAA


AZIM Dewji ambaye ni mwanamichezo imeelezwa kuwa kwa sasa anaendelea vizuri akiwa amelazwa Taasisi ya Mifupa ya MOI na matibabu baada ya kuumia ajalini akiwa njiani kwenda Rufiji katika uwekaji jiwe la msingi mradi wa umeme wa Rufiji, juzi.

Inaelezwa moja ya mfupa wake katika uti wa mgongo umevunjika na anaendelea na matibabu.

Dewji amewahi kuwa mfadhili na mdhamini wa Simba kwa nyakati tofauti 1993, na klabu ya  Simba ilifika fainali ya Afrika na kufungwa na Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Pia amewahi kuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Reginald Mengi ambaye ametangulia mbele za haki.

SOMA NA HII  WOLVES WAMTAKA MMOJA KUTOKA ATLETICO MADRID