Home Habari za michezo MGUNDA AMPA ‘MAKAVU LIVE’ PHIRI KUHUSU UBINAFSI….AMTAKA AACHE KUJIFIKIRIA YEYE TU…

MGUNDA AMPA ‘MAKAVU LIVE’ PHIRI KUHUSU UBINAFSI….AMTAKA AACHE KUJIFIKIRIA YEYE TU…

Habari za Simba

Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC Moses Phiri amefichua mazungumzo kati yake na Kaimu Kocha Mkuu wa klabu hiyo Juma Ramadhan Mgunda.

Phiri amekua mwiba mchungu katika Ligi Kuu Tanzania Bara akifunga mabao matano hadi sasa, huku Kimataifa akifunga idadi hiyo katika michezo minne aliyocheza msimu huu 2022/23.

Mshambuliaji huyo amesema amekua na mazungumzo ya mara kwa mara na Kocha Mgunda kwa ajili ya kuboresha kiwango chake na kuendelea kufunga ili kuisaidia Simba SC kupata mafanikio msimu huu.

Amesema Kocha huyo amekua akimwambia asiwe na Presha yoyote ndani ya Uwanja na badala yake amemtaka acheze kitimu zaidi, kwani mabao yatakuja bila wasiwasi wowote.

“Kocha Mgunda amekua akizungumza na mimi mara kwa mara na nimekua nikifuata maagizo yake, amenitaka nihakikishe kuwa nafunga mabao mengi ya kutosha kwa ajili ya timu ili tuweze kupata mafanikio.”

“Kuhusu mimi binafsi ameniambia kuwa nikicheza kwa ajili ya timu zaidi kila kitu kinakuja, kama kufunga nitafunga zaidi kwa kuwa nafasi zitakuja kutokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzangu, hivyo wala sina presha kwani kila kitu kitakuwa sawa.” amesema Mshambuliaji huyo.

Phiri alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Simba SC mwishoni mwa msimu uliopita akitokea Zanaco FC ya nchini kwao Zambia, na hadi sasa amekua msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ya Msimbazi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAAIVORY...MANGUNGU ASHINDWA KUJIZUIA SIMBA...AFUNGUKA HALI ILIVYO..