Home Uncategorized GWAMBINA YAYEYUSHA POINTI TATU MBELE YA RUVU SHOOTING

GWAMBINA YAYEYUSHA POINTI TATU MBELE YA RUVU SHOOTING

 


KLABU ya Biashara United leo imekubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Pwani.


Gwambina ambayo imepanda daraja msimu huu haijaambulia pointi tatu kwenye mechi zake tatu ilizoanza nazo kwa msimu huu wa 2020/21 zaidi ya kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Gwambina Complex.


Kibindoni ina pointi moja na haijafunga bao hata moja ndani ya dakika 270 huku ikiwa imefungwa mabao mawili baada ya kuanza kupoteza pointi tatu mbele ya Biashara United na leo Septemba 21 imepoteza mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0.


Bao pekee la ushindi kwa Ruvu Shooting lilipachikw dakika ya 41 na Full Maganga na kuwafanya Gwambina wakwame kuweka mzani sawa.


Ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi moja kwenye msimamo huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 10 na pointi zake nne kibindoni zote zimecheza mechi tatu na kukamilisha mzunguko wa tatu kwa msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA MAANGAMIZI CHA NDANDA FC MSIMU WA 2019/20