Home Uncategorized KOCHA MPYA LIPULI ABEBA MATUMAINI MAPYA

KOCHA MPYA LIPULI ABEBA MATUMAINI MAPYA


 KOCHA Mkuu wa Lipuli Nzeyimana Mailo raia wa Burundi amesema kuwa ana imani ataleta mabadiliko ndani ya timu ya Lipuli baada ya kupewa kandarasi ya mwaka mmoja kutokana na kuiona timu kwenye mechi tatu.

Mailo alikuwepo kwenye jukwaa wakati Lipuli ikicheza na Simba, Mbeya City na Tanzania Prisons aikuwa akiifundisha timu ya Framboo ya Burundi amechukua nafasi ya Mrundi mwenzake Harerimana Haruna ambaye yupo na KMC.

“Timu haipo kwenye nafasi nzuri ila kwa muda ambao nimeiona timu nina imani kwamba kuna mambo yatabadilika na timu itapata matokeo, kuhusu kupoteza mechi zake ni sehemu ya mpira kwani hata timu kubwa zinapoteza,” amesema.


SOMA NA HII  REAL MADRID,CHELSEA ZAKUTANA KWA KIUNGO KAI