Home Habari za michezo UWANJA WA YANGA SASA MAMBO NI BAMBAM…GSM KUMWAGA MPUNGA WA MAANA…

UWANJA WA YANGA SASA MAMBO NI BAMBAM…GSM KUMWAGA MPUNGA WA MAANA…

Habari za Yanga SC

Wakati klabu ya Yanga ikiadhimisha miaka 89 tangu kuanzishwa kwake, mdhamini na mfadhili ya klabu hiyo, Ghalib Said Mohamed ameridhia kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa Uwanja wa Kaunda.

Leo Februari 11, 2024 klabu ya Yanga imefikisha miaka 89 tangu kuanzishwa kwakwe rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said akieleza kukubali kwa mdhamini huyo kuridhia kujenga uwanja katika Makao Makuu ya klabu, Jangwani, Jijini Dar es Salaam.

“Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na mdhami na mfadhili wa Yanga, Ghalib Said Mohamed ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujezi wa uwanja wa kisasa wa klabu yetu katika eneo la Makao Makuu ya klabu yetu, Jangwani, jijini Dar es Salaam.”

“Nitumie fursa hii kumshukuru sana GSM kwa dhamira hiyo inayokwenda kutimiza ndoto ya uongozi wangu, kamati ya utendaji na wanachama na mashabiki wa Yanga kwa kuwa na uwanja wetu,” taarifa hiyo ikaongeza;

“Kwa niaba ya uongozi, mashabiki wa Yanga nipende kumwahidi GSM tutampa ushirikiano wote utakaohitajika kuhakikisha tunafanikisha ujezi wa uwanja wetu.”

Yanga inataka kujenga uwanja wake wa kisasa katika eneo lililopo jengo la klabu hiyo na makao makuu mitaa ya Twiga na Jangwani na tayari Serikali imeruhusu Benki ya Dunia kuanza mchakato wa marekebisho ya Mto Msimbazi na kupatikana kwa eneo la ujenzi wa uwanja huo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ awali alisema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan serikali ina mpango wa kuboresha mji na kujenga ramani kubwa ya mji na itakuwa ni faida kwa klabu hiyo.

“Rais Samia Hassan amekubali Benki ya Dunia juu ya mradi wao wa kuurekebisha Mto Msimbazi. Utaruhusu kuwafidia waliokuwa wanakaa eneo hilo na Yanga kujenga uwanja huo kutokana na ramani ya kuvutia iliyoandaliwa. Kutakuwa na mji unaopendeza na wapenzi wa yanga watajenga uwanja wao na wazo lao hilo limekuja wakati mwafaka.”

SOMA NA HII  YANGA WAFANYA KUFRU MKATABA MPYA WA MWAMNYETO...APEWA MIAKA MIWILI YENYE MAMILIONI YA PESA...