Home Habari za michezo A-Z JINSI YANGA WALIVYOMALIZANA NA BEKI KISIKI AKIWA KAMBINI NA TIMU YA...

A-Z JINSI YANGA WALIVYOMALIZANA NA BEKI KISIKI AKIWA KAMBINI NA TIMU YA TAIFA KWENYE CHAN…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa beki kisiki kutoka taifa la Mali, Mamadou Doumbia mwenye umri wa miaka 27 tayari kwa kuwatumikia Wananchi akitokea Stade Malien ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Mali.

Doumbia aliyezaliwa Februari 28, 1995 ana urefu mita 1.88 sawa na futi 6.2 na anasifika kwa kucheza mipira ya kichwa na anatumia zaidi mguu wa kulia.

Timu ambazo amewahi kucheza ni OC Safi, Stade Malien na ana mataji saba ya mashindano mbalimbali.

Doumbia aliisaidia Timu yake ya Taifa kutinga Fainali ya CHAN mwaka 2021 baada ya kuifunga Guinea kwa changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Djigui Diarra aliokoa penati ya tano ya Guinea.

Katika mchezo wa Fainali wa CHAN, Mali wailipoteza baada ya kufungwa na Morocco bao 2-0.

Usajili huo wa Doumbia ni kazi bora ya ushawishi iliyofanywa na kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra ambaye aliposikia mabosi wake wanatafuta beki wa kati basi haraka akawaambia “mleteni huyu jamaa aje awakomeshe.”

Usajili huo unailazimisha Yanga lazima kuondoa jina moja kati ya winga Tuisila Kisinda au kiungo Gael Bigirimana ili kupata nafasi ya kumuingiza Doumbia.

Yanga tayari imeshamsajili kiungo mzawa Mudathir Yahya huku pia wakiwa wamemalizana na mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Mkongomani, Heritier Makambo ambaye ameshaondoka klabuni hapo.

Katika kikao cha kumpa mkataba mpya Diarra ndio usajili huo wa Doumbia ulipochomoza ambapo Diarra aliposikia mabosi wake wakijiuliza katika kusaka beki wa kati ndio alipowatajia mtu huyo mrefu.

Doumbia ni mmoja kati ya mabeki nane ambao wataiwakilisha Mali katika fainali hizo wakiwa kundi D ambapo watacheza mchezo wao wa kwanza Jumatatu Januari 16 dhidi ya Angola.

Doumbia ambaye uimara wake mkubwa ni kuwa na nguvu sambamba na urefu wa futi 6.2 kamili akijua kutumia kimo hicho katika kupambana na mipira ya juu.

Yanga inamtaka beki huyo maalum kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa nao kundi D sambamba na timu za TP Mazembe (DR Congo), US Monastir(Tunisia na Real Bamako (Mali).

Yanga itaanza kampeni hiyo ya hatua ya makundi dhidi US Monastir Februari 12 ugenini kisha wakirudi nyumbani siku 7 baadaye wakiwakaribisha Mazembe kisha wakifunga mzunguko wa kwanza wakiwafuata Real Bamako Februari 26.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTAMBULISHWA..KUMBE USAJILI WA AUCHO HAUJAKAMILIKA..UKWELI HUU HAPA