Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YASHINDA MBELE YA CHIPUKIZI

MTIBWA SUGAR YASHINDA MBELE YA CHIPUKIZI


 MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi ambalo limeanza kufanyika leo Januari 5 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chipukizi kwenye mchezo wa ufunguzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.


Mtibwa Sugar walianza kwa kasi kipindi cha kwanza ila mambo yalikuwa magumu kwao kupata nafasi ya kufunga ambapo dakika 45 za mwanzo sawa na wapinzani wao Chipukizi ambao nao walikuwa kwenye ubora kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili iliwalazimu Mtibwa Sugar kusubiri mpaka dakika ya 58 kushangilia bao lililojazwa kimiani na Mzanzibar Hilika Ibrahim ambaye alipachika bao hilo kwa shuti akiwa ndani ya 18.

Nyota wa mchezo wa leo amechaguliwa kuwa Juma Nyangi ambaye amepewa zawadi ya shilingi laki mbili amesema kuwa ni mwanzo wa timu hiyo kufanya vizuri.


“Kwetu ni mwanzo mzuri na kwa tulichokifanya ni wakati wetu wa kufanya vizuri kwa mechi zetu zijazo, huu ni mwanzo, asante kwa mashabiki, asante kwa wachezaji pia kwa kupambana,” amesema.

SOMA NA HII  HESABU ZA YANGA NI KUIMALIZA KAGERA SUGAR MAPEMA TAIFA