Home Uncategorized YANGA WAIVUTIA KASI JAMHURI, ZANZIBAR

YANGA WAIVUTIA KASI JAMHURI, ZANZIBAR

 


KIKOSI cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuvaana na Jamhuri kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi leo Januari 5.


Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi ni Mtibwa Sugar ambao walitwaa msimu wa 2020.


Mtibwa ilishinda bao 1-0 mbele ya Simba na kufanya iwe imetwaa mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi. 


Timu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina inaongoza kwa kutwaa mataji mengi ya Kombe la Mapinduzi ikiwa imetwaa mataji manne.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck imetwaa taji hilo mara tatu.


Mtibwa Sugar wataanza kwenye mechi ya ufunguzi ambapo watacheza dhidi ya Chipukizi ya Chipukizi, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.

SOMA NA HII  BUNDESLIGA YAREJEA KWA KISHINDO, HAALAD AANZA YAKE