Home Uncategorized MECHI YA SIMBA KOMBE LA MAPINDUZI YAPELEKWA MBELE

MECHI YA SIMBA KOMBE LA MAPINDUZI YAPELEKWA MBELE

 


LEO Januari 5,Kombe la Mapinduzi linaanza kutimua vumbi visiwani Zanzibar na mchezo wa Simba dhidi ya Chipukizi umepelekwa mbele.


Mchezo wa ufunguzi utakuwa ni kwa Mabingwa watetezi Mtibwa Sugar ambao watamenyana na Chipukizi na ule wa pili utakuwa ni kati ya Yanga na Jamhuri.


Kamati ya Kombe la Mapinduzi imesema kuwa mchezo huo ambao ulipaswa uchezwe Januari 7 utachezwa Januari 8.


Wakati mchezo huo ukipelekwa mbele mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Mlandenge umerudishwa nyuma, awali ilipangwa kuchezwa Januari 8 sasa utachezwa Januari 7.


Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi,  AimaƱ Due amesema kila kitu kinakwenda sawa na timu zenye majukumu ya kuwakilisha nchi kimataifa zitawasili Januari 7.


Viingilio Kwenye michezo hiyo ni buku tatu na kile cha juu ni buku kumi.

SOMA NA HII  YANGA HAWATAKI MCHEZO DIRISHA DOGO..... WAJA NA BALAA HILI