Home news BAADA YA KELELE KUWA NYINGI MITANDAONI..GOMES AFUNGUKA SABABU YA SIMBA KUCHEZA OVYO...

BAADA YA KELELE KUWA NYINGI MITANDAONI..GOMES AFUNGUKA SABABU YA SIMBA KUCHEZA OVYO JANA


Kocha Mkuu Didier Gomes, ameweka wazi kuwa benchi la ufundi liliwaelekeza wachezaji kucheza kwa nidhamu na kutumia nafasi zitakazopatikana ili kupata ushindi ugenini na jambo hilo limetokea.

Gomes amesema katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hasa za ugenini unatakiwa kucheza kwa nidhamu kuhakikisha hufungwi bao na kutumia nafasi zinazopatikana ili kujiweka sehemu salama kuelekea mechi ya marudiano.

Gomes amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya na kujitahidi kufuata maelekezo walioyowapa na kusababisha kupatikana kwa ushindi huo umuhimu.

“Unapocheza ugenini siyo lazima kucheza soka la kuvutia badala yake unatakiwa kucheza kwa nidhamu ya kujilinda na kutumia nafasi unazopata kama wachezaji wangu walichofanya leo, nawapongeza sana kwa hilo,” amesema Gomes.

Akizungumzia mabao mawili ya haraka tuliyofunga Gomes amesema ni jambo ambalo tumelifanyia kazi mazoezini na wachezaji wameenda kulikamilisha uwanjani.

“Tuliwatazama Galaxy kupitia mkanda wa video tukawaona wana shida kwenye mipira kona na ya kutenga hivyo tukatumia mapungufu yao kupata mabao,” amesema Gomes.

SOMA NA HII  WAJUMBE WAPYA WA SIMBA WAANZA NA HILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here