Home news KINDA LA AJAX YA UHOLANZI LATUA TZ…WATETA HAYA NA KOCHA WA TAIFA...

KINDA LA AJAX YA UHOLANZI LATUA TZ…WATETA HAYA NA KOCHA WA TAIFA STARS


KIJANA Barka Seif aliyefanya majaribio katika klabu ya Ajax leo Oktoba 18 ametembelea makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Barka alifanya majaribio katika timu ya vijana ya Ajax inayoshiriki Ligi kuu nchini Uholanzi.

Barka alikutana na katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao na kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania, Kim Poulsen na alipata bahati ya kuzungumza nao mawili matatu.

Akiwa katika ofisi za TFF aliambatana na sehemu ya tuzo zake alizozipata katika klabu ya Ajax.

Mchezaji huyo ambaye ni mtanzania wa kwanza kufanya majaribio katika klabu ya Ajax ambayo ni miongoni mwa timu kubwa Duniani.

Barka awali baada ya kumaliza majaribio yake nchini Uholanzi alipata fursa ya kukutana na balozi wa Tanzania nchini humo, Irene Kasyanju.

SOMA NA HII  FT: YANGA SC 4-0 MBEYA KWANZA...HATIMAYE MAYELE KAONA MWEZI...BADO POINTI SITA TU KISHINDO KILIE JANGWANI...