Home news SPOTI XTRA LAMWAGA TIKETI KWA MKAPA

SPOTI XTRA LAMWAGA TIKETI KWA MKAPA

GAZETI la Spoti Xtra jana liligawa tiketi kwa mashabiki Simba katika mchezo wa Tamasha la Simba Day uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar

 Katika tamasha hilo, gazeti la Spoti Xtra lilianda promosheni maalum ya kugawa tiketi kwa mashabiki waliokutwa na Gazeti hilo uwanjani hapo.

 Mkuu wa Idara ya masoko, Juma Johannes alisema kuwa lengo la promosheni hiyo ni kuwaleta mashabiki pamoja kwa kuonyesha namna gani gazeti la Spoti Xtra linawathamini kwa kupata tiketi hizo.

“Lengo kubwa kwetu lilikuwa kupata mashabiki burudani ya kuweza kuangalia huu mchezo wa Simba dhidi y TP Mazembe katika tamasha lao la Simba Day na jambo kwetu limeenda vizuri na tunawapongeza wote ambao wamefanikiwa kupata tiketi za bure kwa kununua gazeti la Spoti Xtra.

 “Kikubwa ambacho tulichokifanya ni kuwapa tiketi wale wote ambao tulikuwa tumewakuta wanasoma gazeti la Spoti Xtra na kwakweli walikuwa ni wasomaji wengi tunaowaomba waendelee kusoma magazeti yetu,” alisema Johannes.

SOMA NA HII  WAKATI IKIWA KARIBU NA KUWEKA HISTORIA MPYA TZ..BACCA NA NABI LAO MOJA YANGA SC...