Home news BAADA YA KUZIBULIWA JUZI..KOCHA WA ASEC AFUNGUKA KILICHOWAPONZA…ATAJA MAKELELE YA SIMBA…

BAADA YA KUZIBULIWA JUZI..KOCHA WA ASEC AFUNGUKA KILICHOWAPONZA…ATAJA MAKELELE YA SIMBA…


KOCHA Mkuu wa Asec Mimosas, Julien Chevalier raia wa Ufaransa, ameukubali muziki wa Simba na kuweka wazi kuwa ameamini wapinzani wao hao kuwafunga wakiwa uwanja wao wa nyumbani, ufanye kazi kubwa sana.

Chevalier alisema mbali ya ubora wa kikosi cha Simba, wamekuwa na nguvu kubwa ya mashabiki ambao amekiri walikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi waliopata.

Juzi Jumapili, Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa, Dar, iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika Kundi D.

Chevalier alisema: “Kusema ukweli Simba walikuwa wanastahili kushinda dhidi yetu kutokana na ubora mkubwa wa kikosi chao na nguvu yao wakiwa wanacheza nyumbani.

“Tulijitahidi kutumia mbinu na mipango yetu, lakini hatukufanikiwa, mashabiki wao walikuwa msaada mkubwa kwao wakiongezewa hamasa.

“Wachezaji wangu wengi vijana, kelele ziliwaathiri kwa sababu wamekaa miaka miwili bila uwepo wa mashabiki viwanjani kutokana na corona.”

SOMA NA HII  BREAKING NEWS: NDOA YA SIMBA NA VUNJA BEI YAISHA....ATAKAYEZALISHA JEZI MPYA HUYU HAPA...