Home Habari za michezo BREAKING NEWS: NDOA YA SIMBA NA VUNJA BEI YAISHA….ATAKAYEZALISHA JEZI MPYA HUYU...

BREAKING NEWS: NDOA YA SIMBA NA VUNJA BEI YAISHA….ATAKAYEZALISHA JEZI MPYA HUYU HAPA…

Habari za Simba

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kumpa tenda ya kutengeneza na kusambaza jezi zake Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited ambao ni wamiliki wa maduka ya Sandaland the only one.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo na kuthibitishwa nasi, zinadai kuwa Uongozi wa klabu hiyo umefikia hatua hiyo mara baada ya Fred Ngajiro kupitia kampuni ya Vunja Bei kumaliza mkataba wa miaka miwili waliosaini hapo awali.

Katika mkataba wa awali , Vunja bei walikuwa wakiipa Simba Bilioni 1 kwa mwaka, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba endapo pande mbili zikiafikiana.

Aidha inaelezwa kuwa chanzo cha Simba kutoamua kuendelea na Vunja bei ni pamoja na changamoto za jezi kucheleweshwa kuja kwa wakati huku ikidaiwa kuwa mmiliki wa Sandaland aliweka dau kubwa zaidi ya lile ambalo Vunja Bei alitaka kutoa.

Taarifa za ndani zinadai kuwa Sandaland watasaini mkataba wa Mwaka mmoja wa kutazamwa ambapo katika kipindi hiko wataipa Simba karibu bilioni mbili ukijumuisha na ongezeko la thamani.

Pia Kulingana na mkataba huo, Sandaland wamepewa haki ya kuisimamia Simba kwenye matukio yake ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mashabiki kununua jezi na kwenda uwanjani.

Mtoa taarifa wetu aligusia pamoja na Sandaland, kuna kampuni moja ya Watanzania ambayo inahusika na kuuza jezi ndani na nnje ya nchi ambao nao walikuwa sehemu ya walioweka ‘Bid’ ya kupewa tenda hiyo.

Aidha kampuni za kimataifa kama Puma ya Afrika Kusini nao pia walituma ofa zaa lakini ukaribu wa mmiliki wa Sandaland na mabosi wa Simba ikawa rahisi dili hilo kuwaangukia wao.

Awali Simba walikuwa wakivaa jezi za Uhlsport ambazo za kampuni ya Kijerumani,ambapo tenda ya kuleta jezi hizo ilikuwa kwa Katibu Mkuu wa zamani wa timu hiyo Kassim Dewji kupitia kampuni yake ya Romario Sports Wear, ambapo alikuwa akiipa Simba Tsh Milioni 150 kwa mwaka mkataba aliousaini kipindi cha Magori akiwa CEO.

Ni katika wakati wa Barbara Gonzalez akiwa kama CEO ndio Fred Ngajiro alipopata nafasi ya kuwa mzalishaji na muuzaji wa jezi na vifaa vya klabu hiyo, kwa mkataba waliousaini Msimu wa 2020/21 ambao umeisha msimu huu wa 22/23.

SOMA NA HII  ACHANA NA BILIONI 2 ZA KUMUUZA LUIS....SIMBA SC WAANDIKA REKODI HII MPYA KWA AL AHLY