Home Habari za michezo AHMED ALLY :- YANGA WANANYANYASA WACHEZAJI WAO…WANAHELA ZA KULIPA WASANII TU…

AHMED ALLY :- YANGA WANANYANYASA WACHEZAJI WAO…WANAHELA ZA KULIPA WASANII TU…

Habari za Michezo leo

Wakati taarifa zikizagaa kuwa Wachezaji wa Yanga Princes (hasa wazawa) wamepanga kufanya maandamano ili kuushinikiza malipo yao baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Wanawake.

Meneja wa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika andiko akionekana kama anawapa mbinu wachezaji hao namna ya kupata maslahi yao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ahmed ameaandika;

Hela za kununua Wasanii si mngewalipa hawa Watoto wa kike?

Kwanini mnawanyanyasa sana? Kwa sababu hawana sauti ndo maana mnawadhalilisha?

Mmewatekelekeza kambini tangu ligi imemalizika May 17 wanaishi hovyo tuu

Mnafanya mambo mengi ya maigizo ili muonekane wasafi kumbe mnanyanyasa wadada wa watu

Misaada mnayotoa si mgeanza kwa kulipa haki za hawa Wadada?

Nimelia sana sijalala usiku kucha baada ya kuona hii taarifa

Poleni UTO Princess halafu msiende Jangwani na nyie pale kuna wauza jezi tuu nendeni Posta ndo mtawakuta”

Wachezaji wa Yanga Princess wanadaiwa kudai stahiki zao ikiwemo mishahara na pesa za usajili kwa baadhi ya wachezaji ambazo hawajalipwa mpaka hivi sasa.

SOMA NA HII  SARE YA SIMBA vs AL AHLY YAMUIBUA MSIGWA AFUNGUKA KUHUSU GOLI LA MAMA