Home Habari za michezo BAADA YA LIGI KUU TZ KUISHA…SportPesa WAMETOA TAMKO HILI KWA YANGA….

BAADA YA LIGI KUU TZ KUISHA…SportPesa WAMETOA TAMKO HILI KWA YANGA….

Yanga na Sportpesa

Wadhamini Wakuu wa Klabu ya Young Africans Kampuni ya Kubashiri Michezo ‘Sportspesa’ wamekiri kufurahishwa Mafanikio ya Klabu hiyo msimu huu 2022/23, huku wakisema Klabu hiyo imetimiza malengo yake na wana deni kubwa msimu ujao.

Young Africans imefanikiwa kutetea mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ huku ikifika Fainali ya Kombe la SHirikisho Barani Afrika dhidi ya USMA Alger iliyotwaa ubingwa wa Michuano hiyo kwa kanuni ya bao la ugenini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Sportpesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema Young Africans wana deni kubwa msimu ujao kuhaki kisha wanalinda na kuyatetea “Kama Sportpesa tunawaahidi Young Africans kuwapa sapoti kubwa na zile bonasi zao zipo pale pale,” amesema Tarimba.

“Sisi kama Sportpesa tumefurahishwa sana na mafanikio ya Young Africans msimu huu, ndani na nje wamefanya vizuri, wamenitimiza malengo yao na yetu, kazi kubwa iliyobaki kwao ni namna ya kuyalinda mafanikio hayo msimu ujao.

“Unapofanya vizuri basi yule anayefanya vibaya anaangalia wapi amejikwaa ili msimu ujao atoe upinzani, hivyo kwa Young Africans ni kujiimarisha zaidi kuhakikisha wanajiimarisha kuliko hapa, nafahamu wana mipango mizuri ya msimu ujao hivyo watafanya vyema pia.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI KUHUSU MORRISON KUTOWEKA SIMBA...HITIMANA AWEKA KILA KITU HADHARANI....