Home news BAADA YA KUISOMA SIMBA…KISINDA KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKATAMKA NENO HILI MOJA TU…

BAADA YA KUISOMA SIMBA…KISINDA KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKATAMKA NENO HILI MOJA TU…


KIUNGO Mshambuliaji wa RS Berkane ya Morocco, Tuisila Kisinda ambaye alikipiga Yanga msimu uliopita, ametamba kuifunga Simba Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mchezo huo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, unatarajia kuwa mkali kwani Simba watakuwa wanataka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-0 na Berkane kule Morocco.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye kundi lao wakiwa na alama 4, huku kinara wakiwa RS Berkane kwa alama 6.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatano, Tuisila alisema kuwa, Simba wawe makini wasije kupigwa na kwao.

“Nitafurahi tena kuweza kuikanyaga ardhi ya Tanzania maana ni nchi ninayoipenda sana, mchezo wetu na Simba utakuwa mgumu sana ninajua hilo ila nitamfunga Simba, Dar.

“Tumejipanga ipasavyo kuweza kushinda, halafu mimi kuifunga Simba sio jambo la ajabu maana hata nilivyokuwa Yanga tulikuwa tunawafunga.”

Berkane walitarajia kuanza safari jana Jumatano huku wakipanga kupitia nchini Ethiopia na baadaye kutua Tanzania.

SOMA NA HII  TAARIFA NJEMA KWA MASHABIKI WA YANGA..HAKIKISHA LEO UNABANDO MUDA WOTE...NCHI ITATETEMA UPYAA...