Home news TAKWIMU ZINAONGEA: SIMBA WAONGOZA MSIMAMO KWA KUKOSA PENATI…YANGA MHHH…

TAKWIMU ZINAONGEA: SIMBA WAONGOZA MSIMAMO KWA KUKOSA PENATI…YANGA MHHH…


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba ,imeingia katika takwimu ngumu wakiwa ndio timu inayoongoza kwa kukosa penalti.

Mpaka sasa Simba imekosa jumla ya penalti 5 huku tatu kati ya hizo wakikosa washambuliaji wao watatu.

Nahodha wa Simba John Bocco pamoja na wenzake Meddie Kagere, Chris Mugalu wameungana na kiungo Rally Bwalya huku beki Erasto Nyoni naye akiwemo.

Biashara wako nyuma ya Simba wao wakikosa penalti mbili kupitia wachezaji wao wawili tofauti Collins Opare na Baron Oketch.

Wachezaji waliokosa penalti mpaka sasa ni pamoja na Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Oketch (Biashara United), Habib Kyombo (Mbeya Kwanza), Boban Zirintusa (Mtibwa Sugar).

Wengine ni Opare (Biashara United), Emmanuel Mvuyekule(KMC), Eliud Ambokile (Mbeya City), Raymond Masota (Geita Gold), Renatus Kisase (Ruvu Shooting), Kagere, Bocco, Bwalya, Mugalu na Nyoni (wote wa Simba).

SOMA NA HII  KIMEUMANA SIMBA...PABLO ATAKA MASHINE MPYA TATU...MATOLA NA HITIMANA HATIHATI KUSALIA...