Home Habari za michezo YANGA WAMKOSHA SAMIA AWAPA NENO LA FURAHA

YANGA WAMKOSHA SAMIA AWAPA NENO LA FURAHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa leo Novemba 5 Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kupitia kurasa zake rasmi za Mitandao ya Kijamii Rais Samia ameandika;

“Hongereni Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Upinzani wenu wa jadi wa zaidi ya miaka 85 sasa ni sehemu muhimu ya burudani yetu. Mnawaleta pamoja na kwa namna kipekee, mamilioni ya Watanzania ndani na nje ya nchi yetu”.

Katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1.

SOMA NA HII  VIINGILIO VYA IHEFU vs YANGA HIVI HAPA