Home Habari za michezo TSHABALALA AFUNGUKA KILICHOWAPONZA SIMBA

TSHABALALA AFUNGUKA KILICHOWAPONZA SIMBA

Nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ameeleza eneo ambalo Yanga waliwazidi ujanja ni kwenye viungo.

Tshabalala amesema, mwalimu aliwapa mpango wao mzuri na wao waliingia nao lakini bahati mbaya Yanga akaja na mpango mwingine tofauti.

“Tulijua Yanga anashambulia zaidi kwa kutumia winga zake lakini yeye akajaza zaidi viungo wa kati, hicho ndo kilituvuruga, mwalimu alijitahidi kupambana nacho lakini mwisho wa siku mpinzani alikuwa bora zaidi akashinda,” alisema Tshabalala.

Yanga wamefikisha alama 21 baada ya kucheza michezo nane ya Ligi Kuu ya NBC wakiwa kileleni huku Simba wakishika nafasi ya tatu wakiwa wamecheza mechi saba.

SOMA NA HII  A-Z JINSI YANGA SC WALIVYOWEKA REKODI YA HESHIMA JANA...DONDOO MUHIMU HIZI HAPA..