Home Habari za michezo KOCHA WA YANGA AWEKA CV HADHARANI, ATOA KAULI NZITO KWA MASHABIKI

KOCHA WA YANGA AWEKA CV HADHARANI, ATOA KAULI NZITO KWA MASHABIKI

Kocha Mpya Yanga Miguel Angel

YANGA SC, imematangaza Miguel Ángel Gamondi, kuwa kocha mpya wa timu hiyo akichukua mikoba ya Mtunisia, Nasreddine Nabi ambaye waliachana naye hivi karibuni baada ya mkataba wake kufikia tamati.

Gamondi raia wa Argentina, anajiunga na Yanga akiwa mzoefu wa kufundisha soka Afrika kwa zaidi ya miaka 20, huku muda wake mwingi akiutumia kufundisha timu za Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika.

Kocha huyo mwenye miaka 56, kabla ya kujiunga na Yanga, timu ya mwisho kufundisha ilikuwa Ittihad Tanger ya Morocco ambapo aliachana nayo Aprili 16, 2022.

Mzaliwa huyo wa Olavarría nchini Argentina, pia ana uraia wa Italia ambapo katika ufundishaji wake, anapendelea zaidi mfumo wa 4-2-3-1.

Akizungumza baada ya kutambulishwa rasmi, kocha huyo alisema: “Mambo Wananchi, mimi ni Miguel Angel Gamondi, kocha kutoka Argentina, nimefanya kazi zaidi ya miaka 20 katika soka la Afrika, nimefundisha timu kama Wydad Casablanca, Mamelod Sundowns, Chabab, Esperance.

“Nilipata mafanikio nikiwa na timu hizo, nina furaha kujiunga na timu kubwa ya Yanga, kwangu naweza kusema ni timu kubwa Afrika, yenye mashabiki wengi.

“Ninaamini tutafanya kazi vizuri na mashabiki, viongozi na wachezaji wote kwa jumla kuleta mafanikio zaidi.

“Nina furaha kujiunga nanyi na tutaonana muda si mrefu. Daima Mbele, nyuma mwiko.”

TIMU ALIZOFUNDISHA

1998–1999 Racing Club de Avellaneda

2000 Al-Ahly Tripoli (kocha msaidizi)

2001–2002 Burkina Faso (kocha msaidizi)

2002–2003 Wydad Casablanca (kocha msaidizi)

2004 Espérance (kocha msaidizi)

2005–2006 Mamelodi Sundowns

2007 Hassania Agadir

2007–2009 Platinum Stars

2010–2011 CR Belouizdad

2011–2012 Ittihad Kalba

2012 USM Alger

2013–2014 CR Belouizdad

2014 Al Urooba

2015–2017 Hassania Agadir (Mkurugenzi wa Ufundi)

2017–2019 Hassania Agadir

2020 Wydad Casablanca

2021–2022 IR Tanger

STORI: JOEL THOMAS

SOMA NA HII  KOCHA WA ASEC MIMOSAS AKUBALI KUWAACHIA YANGA KIFAA HIKI...WARABU WANATAMBUA JOTO LAKE...